Ukimya wa Paul Makonda, Katibu Tawala Arusha Afunguka




Baada ya kuibuka kwa minong’ono na maswali kuhusiana na ukimya wa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda hatimaye Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa ametegua kitendawili hicho kwa kueleza kuwa kiongozi huyo kwa sasa yuko likizo.

Akihojiwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari Global TV Online Julai 26, 2024 Missaile Mussa amesema hana taarifa za ziada tofauti na hizo ya kwamba Makonda yuko likizo na kwamba si jukumu la Katibu Tawala wa mkoa kujuwa nini kinaendelea au kinafanywa na mtu aliyeko likizo.

Siku za hivi karibuni kumÄ™kuwa na minong’ono na maswali lukuki yanayotengeneza sintofahamu na pengine wasiwasi miongoni mwa jamii kuhusiana na ukimya wa takribani majuma mawili (2) wa Mkuu wa mkoa wa Arusha


Nafasi za kazi kila siku Tanzania, Serikalini, Makampuni na Taasisi mbalimbali tembelea website yetu ya Global Publishers muda wote bonyeza hapa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad