UTEUZI Mpya: Rais Samia Atengua na Kuteua Baadhi ya Mawaziri

 

UTEUZI Mpya: Rais Samia Atengua na Kuteua Baadhi ya Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).


Kabla ya uteuzi huu Mhe. Kikwete alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akichukua nafasi ya Jerry Silaa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.


Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambapo kwa sasa nafasi hiyo imechukuliwa na Ridhiwani Jakaya Kikwete.


MBUNGE wa Jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk.


Uteuzi huo umefanyika leo Juni 21, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani.

Uteuzi Mpya wa Mawaziri July 2024


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad