VAR Kuanza Kutumika Mechi ya Simba na Yanga

VAR Kuanza Kutumika Mechi ya Simba na Yanga


Kitaeleweka ni Ubaya Ubwela au Nyie Hamuogopi? Ikiwa zimebaki siku 11 tu kabla ya Simba na Yanga kucheza mechi ya Kariakoo Dabi kwenye Ngao ya Jamii.

Timu hizo zitakutana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam kukata utepe wa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2024-2025, zote zikiwa zimetoka kufanya matamasha yao, Simba Day na Wiki ya Mwananchi kwenye uwanja huo huo.

Sasa, taarifa kutoka TFF ni kwamba huenda majaribio ya teknolojia hiyo ya VAR ikaanza katika pambano la Dabi ya Kariakoo ya Ngao ya Jamii au mechi ya fainali ya michuano hiyo, inayoshirikisha timu nne zikiwamo Azam na Coastal Union zitakazovaana kwanza huko New Amaan Complex, mjini Unguja Zanzibar, siku ya Agosti 8 ambapo jioni yake Kwa Mkapa ndipo Yanga na Simba zitapepetana.

Teknolojia hiyo ya VAR ilianza rasmi kutumika mwaka 2016 na Tanzania itaweka historia ya kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kumiliki teknolojia hiyo na kutumika katika ligi.

“Huenda VAR ikatumika katika mechi za Ngao ya Jamii, kwa ajili ya kuanza majaribio kabla ya kuanza kutumika kwenye Ligi Kuu. Sehemu kubwa ya kuruhusiwa kwa teknolojia hiyo imekamilika, ila inasubiriwa kutolewa taarifa rasmi na mamlaka husika,” kilisema chanzo kutoka ndani ya TFF.

Chanzo hicho kimedokeza kuwa wataalamu waliopewa mafunzo ya kuitumia teknolojia hiyo wakishirikiana na maofisa wengine ndio watakaosimamia shoo katika majaribio hayo, ingawa TFF inafanya siri kwa sasa.

Tangu taarifa ya kwamba VAR itaanza kutumika katika Ligi Kuu ya msimu ujao, baadhi ya wadau wamekuwa na maoni tofauti, wengine wakiamini itasaidia kupunguza dosari zilizokuwa zikichangia kuitibulia hadhi ya ligi hiyo kwa misimu ya hivi karibuni, na wapo wanaona ilipaswa kuwa viwanja vyote na sio Kwa Mkapa tu.

Kuhusu ukweli wa jambo hilo, Mwenyekiti wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi alisema atafutwe Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko, Boniface Wambura ambaye simu yake iliita bila kupokewa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad