Waumini Waeleza Sababu Kupinga Kanisa lao Kiboko ya Wachawi Kufungwa

 

Waumini Waeleza Sababu Kupinga Kanisa lao Kufungwa

Waumini wa kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe, maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge jijini Dar es Salaam wamesema miongoni mwa sababu zinazowafanya kupinga uamuzi wa Kanisa hilo kufungiwa ni huduma za kiroho na uponyaji walizokuwa wakizipata kanisani hapo.


Waumini hao wamefika kanisani hapo asubuhi ya leo Jumapili Julai 28, 2024 licha ya kuwa huduma zimesitishwa, lakini wameendelea kusalia makundi makundi huku wengine wakifanya maombi kabla ya kuanza kupinga uamuzi huo.


Barua ya kufungiwa kwa kanisa hilo imetaja sababu ni kwenda kinyume cha taratibu za usajili.


Barua hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 ambayo Mwananchi imeiona iliwaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dibwe kufunga tawi la kanisa hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad