Kocha wa zamani wa Yanga Afrika ambaye sasa anakamatilia mikoba ya kuinoa Namungo FC, Mwinyi Zahera amekimulika kikosi cha waajiri wake wa zamani na kudai kuwa usajili wa kiungo wa Simba, Clatous Chama ni kwa ajili ya kuwakomoa watu.
Amesema kuna usajili ambao unafanywa kwa ajili ya kuumizana tu kama ilivyokuwa wa Chama kwa sababu hakuona mahitaji ya kiungo huyo kutokana na kuwepo kwa mtu anayefanya vizuri pengine zaidi ya Chama.
Yanga imemsajili Chama akitokea Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja, na anatarajia kukutana na changamoto ya wavhezaji kama Stephani Aziz Ki na Max Nzengeli ambao watakuwa wanacheza nafasi moja ndani ya Yanga ta Miguel Gamondi.
Kwa mujibu wa Zahera usajili wa Chama umefanyika kuumiza roho za watu kutoka kwa mpinzani wao. Usajili ni kitu ambacho msimu uliopita haukuwa nacho na kutakiwa ufanye maboresho.
“Ukiangalia usajili uliofanywa msimu uliopita wa Jonas Mkude, hakutakiwa kwa sababu hakuwa kwenye kikosi cha kwanza lakini amecheza mechi chache. Msimu uliopita kulikuwa na mapungufu nafasi ya kiungo, ilimtaka Chama? Ukiangalia kuna mtu kama huyo na amefanya vizuri,” anasema Kocha huyo aliyewahi kukinoa kikosi cha Wananchi.
Ameongeza kuwa usajili unatakiwa kuangalia mchezaji ambaye huna , mapungufu kwa kusahihisha mapungufu yao kwa kusajili kitu ambacho walikikosa na unamleta mtu atakayekata kiu yao