Yanga Kiboko Sana, Wampa Diarra Miaka Miwili Tena

 

Yanga Kiboko Sana, Wampa Diarra Miaka Miwili Tena

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra raia wa Mali, ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Young Africans SC kwa misimu mawili ijayo.


Diarra ambaye alisajiliwa na kikosi hicho Agosti 2021 akitokea Stade Malien ya nchini kwao Mali, ataendelea kuvaa jezi ya Young Africans hadi mwaka 2027,


Mkataba wa sasa wa Yanga na Diarra ulikuwa unatamatika mwisho wa msimu wa 2024/25, hivyo kusaini mkataba mpya wa miaka miwili unamuweka Diarra mpaka msimu wa 2026/2027.


Ubora wa Diarra akiwa langoni kulinda nyavu zisitikiswe zinajieleza kwani ndiye anashikilia Tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa misimu miwili mfululizo ambayo ni 2021-2022 na 2022-2023.


Pia kipa huyo msimu wa 2023-2024 alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika wa Mali baada ya kuonekana kuwa bora zaidi kuwazidi wenzake wanaocheza ndani ya Afrika kutokea nchini Mali.


Mbali na hilo, Diarra alimaliza Ligi Kuu ya NBC akiwa na clean sheet 14 na kuifanya Yanga kuwa kinara wa timu zilizoruhusu magoli machache zaidi msimu wa 2023-2024 na kubeba ubingwa.


Diarra amekuwa sehemu ya mafanikio ya Young Africans tangu alipojiunga na kikosi hicho ambapo msimu wa 2022-2023 alitufikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku 2023-2024 tukicheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Tayari Diarra amecheza Young Africans kwa misimu mitatu na yote hiyo wameshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC mfululizo sambamba na Kombe la CRDB Bank Federation.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad