Yanga Kuanzia Hatua ya Awali Klabu Bingwa Afrika

Yanga Kuanzia Hatua ya Awali Klabu Bingwa Afrika


Leo Julai 11, 2024 Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) litaendesha Droo ya hatua za awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa msimu wa 2024/25 katika makao yake makuu huko Cairo, Misri.


CAF imezianika timu zitakazoanzia hatua ya kwaza ya awali (first preliminary stage) ya Ligi ya Mabingwa ya CAF ya TotalEnergies 2024-25 na TotalEnergies CAF Confederation Cup 2024-25.


Katika Ligi ya Mabingwa ni vilabu 59 ambavyo vitashiriki, wakati katika Kombe la Shirikisho la CAF vikiwa ni vilabu 52.


TotalEnergies CAF Champions League

Vilabu 5 vilivyo katika nafasi ya juu zaidi katika orodha rasmi ya vilabu bora havitashiriki hatua ya kwanza ya awali (first preliminary stage).


Vilabu 54 vilivyosalia vitacheza kuanzia raundi ya 1 ya awali (first preliminary stage). Yaani vilabu vilivyo na viwango vya kati vinne (4), vilabu vilivyo na nafasi ya chini (14) na vilabu visivyo na daraja yaani non ranked clubs (36) kulingana na viwango rasmi vya CAF.


Pots 5 zimeandaliwa kwa ajili ya vilabu 36 visivyo ranked na vilabu 14 vilivyo katika nafasi ya chini, kwa kuzingatia ukaribu wao wa kijiografia.

Al Ahly

ES Tunis

Mamelodi Sundowns

Petro de Luanda

TP Mazembe.




Kwa orodha hiyo hapo juu, Yanga na Azam ambao wanaiwakilisha Tanzania kwenye CAFCL wataanzia hatua ya kwanza ya awali yaani (first preliminary stage).


TotalEnergies CAF Confederation Cup


Vilabu 12 vilivyo katika nafasi ya juu zaidi katika orodha rasmi ya vilabu (CAF rankings) vitaondolewa kwenye awamu ya 1 ya awali (first preliminary stage).


Vilabu 40 vilivyosalia vitacheza kuanzia raundi ya 1 ya awali (first preliminary stage) ambapo vilabu (3) ni vile vilivyopo nafasi za kati kwenye ranking na vilabu visivyo na nafasi (37) kulingana na viwango rasmi vya vilabu kwa mujibu wa CAF.


Pots 3 kati ya timu 37 ambazo hazijaorodheshwa zimeundwa kwa kuzingatia ukaribu wao wa kijiografia.



Ni timu 5 tu ambazo hazitakuwepo kwenye hatua ya awali kwenye Ligi ya mabingwa kutokana na kuwa nafasi za juu za CAF rankings (hii ni kulingana na kanuni za CAF).


Simba SC

RS Berkane

Zamalek

Asec Mimosas

Enyimba

Stade Malien

USM Alger

El Masry

CS Sfaxien

AS Vita

Sekhukhune utd

FC Lupopo.





Kwa timu za Tanzania, Simba SC pekee itaanzia hatua ya pili wakati Coastal Union ambayo inashiriki CAFCC itaanzia (first preliminary stage).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad