Yanga yanpa 'Thank you' Augustine Okrah



Kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Augustine Okrah, hatakuwa sehemu ya kikosi cha Young Africans msimu ujao 2024-2025.


Nyota huyo ambaye amewahi kuichezea Simba SC msimu mmoja, alitua Young Africans Januari 2024 akitokea Bechem United ya Ghana na kuitumikia timu kwa kipindi cha miezi sita.


Okrah licha ya kucheza Young Africans kwa muda mfupi wa miezi sita, lakini mchango wake umeonekana katika mafanikio ya timu.


Kiungo huyo anaondoka Young Africans akiwa ameshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation msimu wa 2023-2024 na kuwa sehemu ya kikosi kilichocheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari ya Yanga imeelza; "Young Africans SC tunamtakia kila la kheri Okrah katika safari yake ya soka."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad