Yanga Yashtukia Mapema Simba na Azamu Kujichimbia nje ya Nchi...


Yanga ni kama imeshtuka vile. Baada ya kuiona Simba ipo kambini Ismailia, Misri na kusikia Azam FC nayo imeondoka nchini kwenda Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao, nayo fasta imeamua kufanya jambo. Mabosi wa klabu hiyo wakishirikiana na kocha Miguel Gamondi, wameamua kuwaondoa mastaa wa timu hiyo na kuwapeleka nje ya nchi ili kujifua kabla ya kuja kuliamsha kwa msimu ujao wa mashindano wakianza na Ngao ya Jamii.

Hivi unavyosoma ni kwamba, Yanga imebakiza siku mbili tu kabla ya kupaa kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki zaidi ya mbili na kucheza mechi kadhaa za kimataifa kujiweka fiti, ikifuta mpango wa awali wa kujichimbia Avic Kigamboni kama ilivyofanya misimu miwili mfululizo iliyopita.

Uhakika kwa sasa ni kwamba Yanga itaenda kukaa Afrika Kusini kwa siku zisizopungua 18 kujindaa na msimu mpya sambamba na kucheza mechi kadhaa za kirafiki za kimataifa huko Afrika Kusini, ikiwamo mechi maalumu ya michuano ya Kombe la Toyota

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad