Ali Kamwe na Ahmedy Ally Walivyoufanya Utani wa Jadi Kuwa na Heshima na Hadhi




Ukweli ni kwamba hawa washkaji wawili @ahmedally_ na @alikamwe ni "game changers" kwenye soka. Wamesaidia sana kubadili mitizamo ya wale "mashabiki maandazi" waliokua wanaona mpira ni matusi na uadui. Yani ukiwa Simba ukiitania Yanga unamininiwa matusi au ukiwa Yanga ukiitania Simba unaoga matusi.

Mimi kuna wakati nilikua nikitania "Uto" kidogo wazee wa mihemko wanakuja kucomment "we baki kwenye siasa tu, mpira huwezi". Yani hata kwenye utani mtu analeta hard feelings. Nakumbuka pia kuna shabiki wa Uto aliwahi kula kichapo pale kwa Mkapa kisa alishangilia Al Ahly ikicheza na Simba. Yani ilifika mahali utani wa jadi ukabadilika kuwa uadui wa jadi.

Lakini polepole tumeanza kurudi kwenye mstari. Ushabiki wa mpira sio uadui. Tunaweza kutaniana na kurushiana tambo, majigambo na kejeli za mpira lakini tukabaki kuwa ndugu, marafiki, washkaji. Asante sana Semaji la CAF @ahmedally_ na Semaji la Kariakoo @alikamwe kwa kuwafundisha Watanzania maana halisi ya ushabiki wa soka. Mmeufanya utani wa jadi kuwa wa heshima na hadhi. Pokeeni maua yenu

Ameandika GJ Malissa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad