Awesu agoma kurudi KMC "Wamerudisha picha sio mimi"

 

Awesu agoma kurudi KMC "Wamerudisha picha sio mimi"

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji wameipa onyo kali klabu ya Simba SC baada ya sintofahamu iliyotokea juu ya usajili wa kiungo Awesu Ali Awesu (28) akitokea klabu ya KMC FC.


Kamati hiyo imeitaka Simba SC kufuata utaratibu wanapomtaka mchezaji kutoka klabu yoyote ya ligi kuu ya Tanzania na kuacha mazoea.


“Niko fresh… Si ndio wao wameposti? Hawajanirudisha mimi wamerudisha picha waliyopost, kama wanaona mimi mchezaji wao sawa! Kwa sasa naelekea mazoezini (Simba), nikitoka tutaongea," amesema Awesu Awesu.


Awesu aliwahi kunukuliwa akisema hawezi kurudi kule (KMC) na ikitokea hivyo ni bora akaacha kucheza soka.


Simba SC ilitangaza kumsajili kiungo kutoka KMC FC Awesu Ali Awesu bila kukamilisha taratibu ambazo KMC walikuwa wamekubaliana na Simba SC.


Mapema mwezi Julai, Awesu Awesu alitangazwa kuwa mchezaji mpya wa Simba SC, siku chache baadae na mchezaji alitangaza kuwaaga KMC.


Wakati yote hayo yanatokea KMC wao walikuwa kimya mbele ya camera huku wakifanya mchakato wa kumrudisha kimya kimya kwa kwenda kufungua kesi kwenye mamlaka za mpira nchini.


Madai ya KMC ni kwamba Simba walitakiwa kupitia kwao ili kujadili thamani ya mchezaji ili wauziwe wakidai kuwa Simba wamepitia kwa mchezaji tu, taarifa za upande wa mchezaji zinaeleza kuwa mchezaji alivunja mkataba kwa kulipa kiasi cha pesa anachotakiwa kulipa kwa mujibu wa mkataba baada ya happ akawa huru ndipo Simba wakamsajili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad