Coastal Union Yamtimua Kocha wao David Ouma

 

Coastal Union Yamtimua Kocha wao David Ouma

Timu ya Coastal Union imeachana na kocha wao David Ouma raia wa Kenya, Ouma na Coastal wamefikia makubaliano ya pande mbili.


Joseph Lazaro na Ngawina Ngawina ndio ambao wamepewa jukumu la kukinoa kikosi cha Coastal Union, wakati wanatafuta kocha mwingine.


Ouma alipewa maelekezo ya kuachia timu ambayo ipo kwenye maandalizi ya mechi ya marudiano ya Kombe ya Shirikisho Afrika jijini Dar es Salaam na kusafiri hadi Tanga kwa ajili ya mazungumzo kutokana na performance mbaya kwenye mechi ya kwanza ya Shirikisho dhidi ya FC Bravos do Maquis ya Angola ambapo mchezo wa marudiano utapigwa keshokutwa Agosti 25, 2024 jijini Dar es Salaam.


Msemaji wa Club ya Coastal Union, Abbas El Sabri amesema; “Kinachoendela ni kwamba, mara baada ya mchezo kule Angola matokeo hayakuturidhisha, yalitusikitisha kwa hiyo wazee wetu pamoja na viongozi wakasema kabla hatujaelekea kwenye mchezo wa marudiano, wanataka kujua nini kilitokea tukapoteza kwa mabao mengi kiasi kile. Mhusika wa moja kwa moja alikuwa mwalimu David Ouma ambaye anaweza kueleza nini kilitokea.


“Wazee na viongozi wakasema Mkuu wa benchi la ufundi aelekee Tanga kwa ajili ya kuzungumza nao ili wajue nini kifanyike ili tushinde mchezo unaofuata. Wachezaji wamesajiliwa kwa gharama kubwa na uwekezaji ni mkubwa lakini haikuakisi matokeo tuliyoyapa. Ndiyo maana tunataka uwekezaji uendane na matokeo yetu uwanjani.


“Malengo yetu ni kufika hatua ya makundi lakini hatuwezi kufika huko kama tunaruhusu mabao kwenye mechi kama ile. Tunachokifanya ni kuziba magepu ili tuweze kutimiza malengo yetu.


“Hatima ya Ouma iko mikononi mwa uongozi ambao wamemwajiri. Kwa vile sasa hivi akili yetu ipo kwenye mechi, mechi ikimalizika ndipo kitafahamika kwa sababu matakwa yetu sisi ni ushindi.


“Benchi la ufundi halina mtu mmoja, lina watu wengi kwa hiyo kama yeye hayupo basi Ngawine Ngawine ambaye ni kocha msaidizi anachukua majukumu. Kuwepo kwake au kutokuwepo kwake sio tatizo sana, wapo wasaidizi ambao wanaweza ku-cover na hamna tatizo,” amesema Abbas.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad