Dada wa Kazi Aliyemkata Mtoto Shingo Aburuzwa Mahakamani

 

Dada wa Kazi Aliyemkata Mtoto Shingo Aburuzwa Mahakamani

MSICHANA anayefanya kazi za ndani, Clemensia Milembe (19) na mwenzake wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kusababisha kifo.


Ilidaiwa mahakamani kuwa Clemensia ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani katika maeneo ya Goba, alimjeruhi mtoto Maliki Kitumbi kwa kitu chenye ncha kali na kumsababishia maumivu makali katika maeneo ya shingo.


Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Elizabeth Makori maarufu kama mama Brayan anayedaiwa kuhusika katika jaribio hilo.


Wakili wa serikali, Rhoda Kamungu aliwasomea washtakiwa hao mashitaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalila. Kamungu alidai kuwa Julai 15, mwaka huu katika eneo la Kinzundi Goba Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam washtakiwa walijaribu kusababisha kifo kwa Maliki.


Aliieleza mahakama kuwa kitendo walichokifanya ni kinyume na kifungu namba 211 (a) cha sheria ya makosa ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad