"Mimi Sio Mfanyakazi Wa Yanga Na Sipati Hata shilingi Kutoka Yanga, hata Kwenye Mfumo Wa Mishahara Ya Wafanyakazi Wa Yanga Mimi Sipo
Mimi Nina Biashara Zangu Binafsi Ndio Ambazo Zinaniingizia Kipato Na Sio Yanga,pale Yanga Mimi Ni Rais Wa Klabu Na Sio Mfanyakazi Wa Klabu, Mfanyakazi Kazi Wa Klabu Anaanzia CEO Hapo Ndo Level Ya Wafanyakazi Ndani Ya Klabu Yetu Inaanzia"
"Kama kuna jambo ambalo Wanayanga wanapaswa kuliombea DUA liendelee ni uwepo wa GSM kwenye timu yetu, amekuwa akitusapoti katika mambo mengi mno.
Mfano juzi kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuwashughulikia watu fulani, alikuja na kutuuliza bajeti ya Bonasi ikoje, tulipomwambia akasema haitoshi, akaongeza fungu la maana vijana wakaenda kupambana tukashinda" Rais wa Young Africans SC,
“Zile goli 5 tulizoshinda Msimu uliopita zilitupa wakati mgumu sana. Wapinzani walikuwa wanakuja kwenye mechi zetu wakikamia kwa ajili ya kuzuia wasifungwe goli 5 na hiyo ilifanya mechi zetu kuwa ngumu sana.
“Tulichofanya msimu huu ni kuongeza ubora kwenye kikosi chetu, hivyo mtu akizuia sana asifungwe goli 5 anapata kichapo cha goli 4”
“Kila unapoona Wanayanga wanakunywa supu, ujue ni maadhimisho ya zile goli 5. Nimemwambia Ally Kamwe zoezi hili liendelee kwa sababu linatukumbusha tukio lililotupa raha sana mashabiki wa Yanga”