Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewajibu wanasema kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Clatous Chama hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Muargentina huyo.
Gamondi amesema hayo baada ya Yanga kupata ushindi wa bao 4-1 kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Azam FC huku Chama akitoa pasi ya bao la nne lililofungwa na Clement Mzize.
“Sipendi sana kuzungumzia mchezaji mmoja mmoja, wachezaji wote wamecheza vizuri lakini Boka ameonesha ana uwezo wa kucheza ndani ya Yanga. Sio rahisi kwa mchezaji mpya anaingia kwenye timu kama Yanga, hajui mfumo wala mazingira ya timu, ameonesha uwezo mkubwa kwenye mechi dhidi ya Simba na leo dhidi ya Azam alikuwa bora sana.
“Chama sihitahi kumzungumzia sana, ninamheshimu ni mchezaji mkubwa na mzuri lakini kama ambavyo nimekuwa nikisema, wachezaji wote ambao ni wapya wanatakiwa kupamba ili wapate nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
“Wachezaji wapya nimekuwa nikijaribu kuwapa nafasi kidogo kidogo ili kuona uwezekano wa kuwa wanaanza lakini hii ni professional football, tunahitaji kuonesha uwezo, mchezaji anaonesha uwezo atapewa nafasi kwa sababu tunahitaji kushinda na kupata mataji,” amesema Gamondi.