HARMONIZE ashindwa KESI, atakiwa kuilipa CRDB mamilioni baada ya kushindwa kurudisha MKOPO

HARMONIZE ashindwa KESI, atakiwa kuilipa CRDB mamilioni baada ya kushindwa kurudisha MKOPO


HARMONIZE ashindwa KESI, atakiwa kuilipa CRDB mamilioni baada ya kushindwa kurudisha MKOPO

Msanii wa muziki wa Bongofleva Rajab Abdul alimaarufu kama Harmonize atakiwa kuilipa Benki ya CRDB fidia ya Millioni 10, gharama za kesi na Deni la Mkopo la Tsh. Milioni 103 baada ya kushindwa kulipa kikamilifu Mkopo wa Tsh. Milioni 300 tokea Mwaka 2019

CRDB na Harmonize walikubaliana angefungua akaunti ya Kibiashara katika benki hiyo kisha kuweka Tsh. Milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za Kibiashara, lakini alikiuka makubaliano hayo.

Benki ya CRDB ilifikia uamuzi wa kwenda Mahakamani baada ya usumbufu wa ulipaji deni kutoka kwa msanii

huyo, ambapo Mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Msanii huyo lakini hakufika Mahakamani.

Harmonize anatakiwa kuilipa Benki hiyo kiasi cha milioni 103 kutokana na mkopo aliyouchukua katika benki hiyo na kushindwa kulipa kwa kuzingatia makubaliano yaliyowekeana na Benki hiyo.

Tazama VIDEO:




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad