Hizi Hapa Mechi Zote za CAFCL Raundi ya pili, Wakubwa Wamerejea

 

Hizi Hapa Mechi Zote za CAFCL Raundi ya pili, Wakubwa Wamerejea

Baada ya mchezo wa pili wa marudiano wa michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) hatua ya awali young Africans SC imevuna kiasi cha Milioni 30 za goli la Mama.


Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi ya Milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) maarufu kama "goli la Mama".


Mchezo wa kwanza Young Africans SC ilivuna kiasi cha Milioni 20 baada ya kupata ushindi wa magoli 4-0 na leo wamepata Milioni 30 baada ya kushinda magoli 6-0 na kufikisha jumla ya Milioni 50 baada ya kufunga magoli 10-0.


Young Africans SC imejinasibu kuwa wataendelea kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ili kuvuna fedha nyingi za goli la mama.


Tanzania ilikuwa na uwakilishi wa timu nne kwenye CAFCL na CAFCC, Yanga SC, Azam FC, Simba Sports Club na Coastal Union. Hadi sasa timu mbili za Azam na Coastal Union, zimeshatolewa.


Hizi hapa timu ambazo zitacheza hatua inayofuata ya CAFCL



Michezo muhimu ya kuangalia katika Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho raundi ya pili:


◉ Al Ahly v Gor Mahia

◉ Piramid v APR FC

◉ TP Mazembe v Red Arrows

◉ Orlando Pirates v Jwaneng Galaxy

◉ MC Alger v US Monastir

◉ Al Hilal v San Pedro

◉ Raja v FC Samartex

◉ Petro Luanda v Maniema

◉ Mamelodi Sundowns v Mbabane Swallows

◉ Al Merriekh v AS FAR / Remo Stars

◉ ASEC Mimosas v ASC Kara

◉ USM Alger v Stade Tunisia

◉ AS Vita Club v Stellenbosch

◉ Nsoatreman v Constantine

◉ Enyimba v Etoile Filante

◉ CBE vs Young Africans

◉ Simba SC v Al Ahli Tripoli


Kwa Yanga hii unadhani itavuna kiasi gani kwenye goli la Mama kimataifa?

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad