“Jambo Afande,
Kuna video nimeiona ya polisi anapiga hiphop on stage Shinyanga nikafurahia sana. Kuna jinsi waliokuwepo wamefurahi sana na kuona huyu ni wetu huyuu. Hivi upolisi ulianzaje kwani? Labda tukijua hili tunaweza kujua jinsi ya kuwa miongoni mwa majeshi ya polisi bora kabisa duniani.
Watu walipoanza kuwa wengi kwenye eneo moja, ilipelekea wengine kuwa wadanganyifu kwa kuiba mavuno ya wengine nk. Baadae wakaja wezi wakubwa zaidi, wanaiba himaya wanaiba ardhi. Flani na flani na flani wakasema “Jamani ehh sisi hapa ndo tuna nguvu, tunajitolea tutalinda ila nyie mtatugawia kidogo kwenye mavuno yenu tuishi”.
Ikafika wakati watu wanaiba kwa makundi makubwa bila kuogopa polisi na polisi wanauwawa. Wakasema “Hapa sasa inabidi tuwe na mapolisi special wa kupiga haya makundi makubwa haya, tuwape jina wanajeshi”. Kwa dhana hii ya juu juu tu, unaona jinsi polisi walivyokuwa kiungo kinachopendwa na kuaminika sana sababu akiwepo polisi wewe una uhakika wa amani unaendelea zako na mishe zako.
Vitabu vingi vikubwa leo ukisoma vinaongelea heroes ambao karibia 95% ni jeshi la ulinzi au wananchi. Ilikuwa mtu anapewa tuzo ya juu kabisa kwa uwezo wake wa kulinda wananchi. Majemedari yalikuwa yanarudi kutoka vitani yanapokelewa kwa sherehe la maana, nchi nzima inasimama kuipokea miamba imerudi. Raha sana.
Sasahivi polisi ni kiungo kilichoingiliwa na sana na wasiopenda upolisi. Kila mmoja wetu ana polisi ambae ni mshkaje wake anatamani polisi wote wangekuwa hivyo. Naamini haya maneno polisi mnayaona na mna jambo dogo sana la kufanya kuchukua imani kamili ya wananchi kwasababu nyie ndo amani yetu ila tuna hofu saaaaaana yani sana tukiwaona tuu bila hata kuwa na kosa.
Katika kujenga taifa,
Mshkaji wenu mliye ishi nae sana.