KUTOKA KWA RAIS WA YANGA ✅
Raisi wa Yanga Injinia Hersi said amekiri kuwa haikuwa rahisi kumsajili kiungo wao mshambuliaji Clatous Chama maarufu kama (Mwamba wa Lusaka)
Hersi amesema Chama ni moja ya wachezaji bora zaidi waliowahi kutokea katika ligi kuu Tanzania Bara kwani levo yake ni kubwa sana kwenye timu, huku akisema kuwa wale wanaosema Chama ni maji ya jioni ni wale wanaommezea mate baada ya kuwaacha
“Moja kati ya wachezaji ambao nilikuwa navutiwa nao katika nchi hii, waliowahi kucheza kwenye ligi kuu ya Tanzania ni Clatous Chama. Ni moja kati ya wachezaji bora, kiwango alichokuwa nacho na mchango wake kwenye timu ni mkubwa sana”
“Hii ni heshima kubwa kwa mchezaji kama huyo kuja kucheza Young Africans, na haikuwa rahisi pia kumleta. Kwahiyo tusidharau hiki kitu kwa kutuambia eti Chama ni mzee sijui maji ya jioni hizi ni kauli tunazijua sizitaki mbichi hizi,” alisema Hersi
Pia Hersi ambaye amekuwa sehemu kubwa ya mafanilio ya Yanga tangu alivyoingia katika klabu hiyo amesema kuwa dhamira yao ni kuona wanatwaa mataji kwa kila mashindano wanayoshiriki
Hersi amesema wanaweza kuwa timu ya kwanza kuleta kombe la Afrika nchini
“Dhamira yetu ni ile ile kama Yanga, kila mashindano tunayoshiriki tunataka kubeba kombe, kwahiyo klabu bingwa tukiweka mguu Jumamosi dhamira kubwa na kwa baraka za mwenyezi Mungu kwanini tusiwe timu ya kwanza kuleta kombe la Afrika hapa Tanzania? Hayo ndio malengo yetu,” aliongeza
Kesho Jumamosi August 17 Yanga itatupa karata yake ya kwanza katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Vital’o ya Burundi katika uwanja wa Azam Complex
Vijana wa kocha Miguel Gamondi leo watakamilisha maandalizi kuelekea mchezo huo na dhamira yao ni kupata ushindi mnono ili kujihakikishia kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi za klabu"