Jeshi la Polisi Lamshikilia Aliyesambaza Habari Kuwa Binti Aliyebakwa Amefariki Dunia


Jeshi la Polisi Lamshikilia Aliyesambaza Habari Kuwa Binti Aliyebakwa Amefariki Dunia

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta Wazo wilaya ya Kinondoni mkoani humo, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa binti mkazi wa Yombo Dovya ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na vijana watano kuwa amekutwa tayari kashafariki dunia.

Kamanda Muliro amesema binti huyo anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai hajafa, kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na kwamba uchunguzi wa tukio hilo la kikatili bado unaendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad