Kama Refa Angekuwa Makini, Simba Wangepigwa Tano Tena - Mchambuzi

 

Kama Refa Angekuwa Makini, Simba Wangepigwa Tano Tena - Mchambuzi

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Azam TV, Dominick Salamba amesema kuwa asingwekuwa mwamuzi wa kati, Hery Sasii kuwabeba Simba basi wangefungwa bao tano na watani zao Yanga kwenye mchezo wa jana.


Salamba amesema hayo baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Yanga kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii, mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo Simba wakifungwa na Yanga.


"Tusitake kujificha kwenye kichaka cha waamuzi wa leo kwa kuangalia tukio moja la mwisho, maana kama wangekuwa makini basi Yanga angeshinda mabao 5 katika mchezo wa leo (jana), mawili yalishazama, penati 1 na offside za mchongo kama 3, Yanga ni above level kwa Simba sasa, wajipange hakuna namna.


"Ile dhana ya mechi ya Simba sc na Yanga sc haina mwenyewe imepitwa na wakati sasa hivi timu iliyo Imara na Bora ndio itakayoshinda hata mara 100, Yanga wanaifunga Simba mara 3 mfululizo na huku wakiitawala Pakubwa,hakuna mchawi zaidi ya kuwa na timu imara na bora," amesema Salamba.


Unakubaliana na maneno ya Mchambuzi?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad