Kipa Camara: Tumaini Jipya la Simba Langoni Baada ya Manula

 

Kipa Camara: Tumaini Jipya la Simba Langoni Baada ya Manula

Simba imepata kipa la maana Mousa Camara, aliyewafanya mabosi wa klabu hiyo kupata jeuri hata kudiriki kumpuuza kipa wao aliyewaheshimisha miaka ya karibuni Aishi Manula.


Camara amekuwa mchezaji wa 14 kusajiliwa Simba kati ya 15 kama atangazwa mshambuliaji mpya, ambapo mechi tatu tu zikatosha kuthibitisha kwamba wekundu hao wamepata kipa wa boli.


Kipa huyu amecheza dakika zaidi ya 40 kwenye mechi ya Simba day dhidi ya APR, kisha akacheza mechi zote mbili wekundu hao walipokuwa wanawania ngao ya jamii msimu huu dhidi ya Simba na Coastal Union na mashabiki kuona ubora wake.


ANACHEZA KROSI, HAFUNGIKI KIRAHISI


Kwenye mechi hizo tatu ambazo Camara amekaa langoni ameonyesha ubora mkubwa wa kucheza krosi nzito tena kwa utulivu mkubwa akiwa na kikosi hicho cha wekundu hao.


Mbali na kucheza huko krosi hesabu za Camara akiwa langoni ni kubwa sio kirahisi unaweza kutikisa nyavu za timu hiyo akijua kucheza na miguu na mikono yake.


UREFU SAFI


Ubora mkubwa wa Camara kucheza mipira ya juu ukiacha ufundi wake lakini amesaidika kutokaana na urefu wake wa futi sita na nchi moja alionao ambao umemfanya kuwa imara kwa mipira ya juu akiweza kucheza vizuri mashambulizi ya juu.


MGUUNI MTU


Ubora mkubwa uliombeba kipa wa Yanga Djigui Diarra ni ubora wake wa sio tu kuwa kipa kwa kujua kudaka lakini, ubora wa umiliki wake mpira miguuni, hana presha mpira ukija ba Camara naye yumo anga hizo.


Ile mechi dhidi ya Coastal Union kumbuka alipompa ‘kanzu’ mchezaji wa timu hiyo kisha alipokuja mwingine akampunguza kwa chenga safi na kulifanya jukwaa ‘kutapika’ kutokana na kontroo yake miguuni.


HAWA KAZI WANAYO


Haitakuwa rahisi kwa Camara kukaa benchi kutokana na daraja la ubora alilonalo labda makocha waamue kumpunzisha au aumie.


Makipa wa Simba Ayoub Lakred (inayeelezwa anaondolewa katika system ya usajili, kumpisha straika mpya), Manula na Ally Salim watakuwa na kazi kubwa kujipanga ili kushindana nafasi na raia huyo wa Guinea.


SIO WA ZILE SABA


Ujio wa Camara ulikuja ghafla baada ya kudaiwa Lakred ameumia pamoja na kuongezeka uzito, alipofika baadhi ya mashabiki wakaanza kuchanganya mambo wakidhani huyu ndiye Camara aliyepigwa mabao 7-0 na Simba kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Hata hivyo, ni kweli Camara huyu alikuwa Horoya wakati Simba inaishushia timu hiyo kipigo kikali lakini jamaa alikuwa kama amechungulia, hakuja nchini wakati timu yake inakuja nchini akiwa kwenye adhabu.


Kipa aliyepigwa kipigo hicho alikuwa Mohammed Camara ambaye amesajiliwa na Singida Black Stars msimu huu wakati huo wote wakiwa pale Horoya AC.


YANGA YAMTIBULIA


Camara hata hivyo ameanza msimu kwa rekodi mbaya akipoteza ngao ya jamii timu yake ikivuliwa ubingwa na watani wao Yanga kwa bao moja pekee, lakini licha ya kufungwa akawaachia matumaini mashabiki wa timu yake kufuatia kiwango bora alichoonyesha kwenye mechi hiyo ya nusu fainali.


Huyu ndiye Camara ambaye anaweza kuja kuwa mmoja wa makipa bora wa msimu ujao watakaowania au kutoa ushindani kwenye tuzo ya kipa bora wa msimu ujao.


MATAJI KIBAO


Akiwa na AC Horoya tangu 2025, kipa huyo ametwaa mataji manne ya Ligi Kuu ya Guinea, misimu ya 2015-2016-2016-2017, 2017-2018 na 2018-2019, FA matatu 2016, 2018 na 2029 na mawili ya Super Cup 2017 na 2018, ikiwa na maana kama Siomba itamtumia vyema huenda akaendeleza kismati chake cha kubeba mataji akiwa na Wekundu wa Msimbazi. Acha tuone.


Alikopita: FC Kolombada, Milo FC, AC Horoya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad