Kituo cha LHRC Wamtaka Rais Samia Kukemea Tukio la Msichana Kubakwa

Kituo cha LHRC Wamtaka Rais Samia Kukemea Tukio la Msichana Kubakwa


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa tamko kali dhidi ya kitendo cha kikatili cha unyanyasaji wa kijinsia (kubakwa na kulawitiwa) kilichoripotiwa kumuhusu Msichana mmoja kutoka Dar es Salaam, Wilaya ya Temeke, Kata ya Makangarawe, Mitaa ya Msakala na Dovya, karibu na Shule ya Msingi Yombo Dovya ambapo kimemomba Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kama Mama na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi kutoka hadharani na kuonesha kuchukizwa na jambo hilo.


Akiongea Jijini Dar es salaam leo August 05,2024, Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Anna Henga “Msichana huyu amebakwa na kulawitiwa na Vijana watano waliodai kuwa ni Askari wa moja ya vikosi vya ulinzi Tanzania, kama wanavyojieleza katika video hizo tatu tofauti, Askari hao walimrekodi wakiwa wanamfanyia vitendo hivyo vya kikatili na kusambaza video hizo mitandaoni kwa maagizo ya kiongozi wao (Afande) ambaye aliwatuma kumpatia adhabu”


“Kwa mujibu wa maelezo ya Askari hao, kosa la Msichana huyu ni kutembea na Mume wa bosi wao (Afande), LHRC kama sehemu ya Jamii ya Watanzania tumehuzunishwa na ukatili huu

tunataka Wahusika wote watano na aliyewatuma kulingana na maelezo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria, Jeshi letu la Tanzania ni Jeshi lenye heshima Afrika na duniani lihakikishe linajitenga na kashfa hii ya ubakaji wa Raia wake ambao lina jukumu la kuwalinda (kama kweli Wahusika ni Wanajeshi)”


“Tunapenda pia kutoa pongezi kwa Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa Ubungo, Dar es Salaam, kwa kutoa taarifa hizi, tunapongeza Jeshi la Polisi na Waziri Dorothy Gwajima kwa hatua za awali walizochukua, tunakemea vikali Wahusika wa kitendo hiki na tunawaasa Wananchi kuacha kusambaza video hizo kwenye mitandao ya kijamii ili kumlinda Msichana huyo”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad