KIUNGO wa Simba Fabrice Ngoma Aomba Kuondoka

 

KIUNGO wa Simba Fabrice Ngoma Aomba Kuondoka


KIUNGO wa Simba Fabrice Ngoma, ameonyesha kuto pendezwa na utaratibu wa uongozi wa benchi la ufundi la klabu ya Simba SC, kumuanzisha benchi mchezaji huyo Kila mechi.

Hayo yamezungumzwa kupitia wakala wa mchezaji huyo wakala wa mchezaji Fabrice Ngoma, amesema nibora uongozi wa klabu hiyo useme kama hawana uhitaji naye Kwa sasa Kisha wamlipe pesa ya mwaka mmoja uliobaki Ili aende akatafute changamoto mpya sehemu nyingine.

“Viongozi wa Simba wanamkosea heshima mchezaji wangu,Kama hawamtaki wanipigie Simu ili nimpeleke sehemu Nyingine,kuna vilabu zaidi ya 200 vinamtaka Ngoma,hivyo watulipe hela ya msimu Mzima tuondoke zetu,” amesema fausty world Wakala wa Fabrice Ngoma.

Mechi zote mbili za Kimashindano za Simba, Ngoma ameanzia benchi,  kwenye mechi ya Yanga na Coastal Union ambapo mechi hiyo alioneshwa kkadi nyekundu ambayo itamkosesha mchezo wa kwanza wa Ligi.

Fabrice Ngoma alianza kwenye mchezo wa Simba Day dhidi ya APR na baadae kutolewa nafasi yake akaingia Debra Fernandes Mavambo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad