KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameonekana kutofurahishwa na namna ambavyo Shirikisho la Soka Afrika CAF, linavyopanga ratiba zake ukizingatia michuano ya kimataifa na ile ya ratiba ya kalenda ya FIFA.
Gamondi akizungumzia juu ya mchezo wao wa hatua yapili kufuzu makundi ya Klabu Bingwa Afrika, dhidi ya CBE ya nchini Ethiopia alisema kuwa timu yake ya Yanga inapaswa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.
“Tuna wachezaji 14 wameitwa timu zao za taifa hivyo siwezi kujiandaa mechi yetu ya CAFCL, maana wanarudi siku mbili hadi tatu kabla ya mechi.”- Gamondi.
“Siifahamu timu ya CBE SA ila tunapaswa kupata matokeo mazuri Ethiopia na tuje tufuzu tukiwa hapa Tanzania.”- Gamondi
“Nawashauri CAF sio vizuri kuweka Kalenda ya FIFA na hapo hapo ifuatiwe na michezo ya CAF Champions League, wachezaji wanasafiri sana, wanacheza mechi nyingi, mfano sisi tunacheza Ethiopia 🇪🇹 najua wachezaji wangu watakuja kule ila sio kwenye muda sahihi.”- Gamondi
“Sijajua kwanini CAF hawaliangalii hili, sio sisi tu timu nyingi Afrika zina wachezaji wazuri wanaitwa timu za taifa kama ilivyo kwa Mamelodi Sundowans.”- Gamondi