Kocha Gamondi Ampa TANO Mchezaji Cloutas Chama

 

Kocha Gamondi Ampa TANO Mchezaji Cloutas Chama

KOCHA MIGUEL Gamondi amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Clatous Chama aliyeanza katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa kutoka Simba katika mchezo huo dhidi ya Vital’O ya Burundi na kuasisti na kufunga bao wakati Yanga ikishinda 4-0.

Kocha huyo alisema, Chama ni mchezaji mzuri na mzoefu wa michuano ya Afrika hivyo, licha ya presha kubwa iliyopo juu ya kumtumia mara kwa mara mchezaji huyo, anachozingatia ni weledi.

“Kila mchezaji hapa ana nafasi sawa na wengine ya kucheza kikosi cha kwanza kwa sababu tuna wachezaji bora katika maeneo yote uwanjani na hiki ndicho kiwango ambacho tumekitengeneza kwenye timu iwe ni kwa kipindi kirefu au kifupi,” alisema Gamondi.

Gamondi aliongeza, mashabiki watarajie makubwa kwa mchezaji huyo huku akisisitiza uwepo wake ndani ya kikosi cha Yanga ni muhimu kutokana na mahitaji ya timu hiyo, ambayo malengo yake ni kushinda mataji mbalimbali inayoshiriki msimu huu.

Katika mechi hiyo Chama alimtengenezea nafasi Dube kwa kisigino kabla ya kufunga bao la pili kipindi cha pili na Mzize kuongeza la tatu na Aziz Ki akafunga kwa penalti dakika za lala salama na kumfanya Mzambia huyo kuendeleza rekodi katika mechi za CAF, kwani akiwa na Simba aliiwezesha kutinga robo fainali mara tano, akifunga mabao 15 na kuasisti sita katika mechi 44 alizoichezea tangu ametua kikosini hapo.

Chama alijiunga na Simba Julai Mosi, 2018, baada ya kuachana na Lusaka Dynamos ya kwao Zambia na msimu uliopita katika makundi alifunga bao moja na kuasisti moja Simba ikitolewa na Al Ahly ya Misri.

Rekodi nzuri kwake katika Ligi Kuu Bara ni za msimu wa 2022/2023 alipohusika katika mabao 18.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad