Mastaa Wacharuka, Waingilia Kati Sakata la ‘Waliotumwa na Afande’

 

Mastaa Wacharuka, Waingilia Kati Sakata la ‘Waliotumwa na Afande’

Mastaa wacharuka baada ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya kusema uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi, na yule dada alikuwa kama anajiuza.


Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za mastaa mbalimbali nchini wamechapisha taarifa za kukemea vitendo hivyo na kutaka haki itendeke. Kwa upande wake mwanamuziki Shilole amelitaka jeshi la polisi kutotoa taarifa nusunusu na zisizo nyepesi.


"Haya ni 'kahaba' ndiyo abakwe?. Juzi Mandojo kauliwa tukaambiwa alijificha kibanda cha Mbwa, mbona kama wenzetu mnatoa majibu mepesi sana kujibu vitu vigumu?. Ushauri wangu, angalieni sana maneno ya kusema wakati watu wanalia.


Kama sisi hatumjui yule dogo tunaumia hivi, mmemuwaza mamaake? na ndugu zake? Ndugu zangu Polisi kwa unyenyekevu mkubwa sana niwaombe hili jambo kwa lilivyokaa na yote yaliyoongolewa, angalieni jamani msijeonekana kuna mtu mnamlinda. Msitupe taarifa nusu nusu,"ameeleza Shilole.


Aidha kwa upande wake Lady Jaydee ameomba jeshi la polisi kuwahisha hatma ya tukio hilo. "Tunaomba msaada kuwahishiwa hatma ya hili jambo. Roho za wanawake zinavuja damu. Je ni nani yuko salama dhidi ya ukatili?,"ameleza Jide. Aidha kwa upande wake mwanamuziki wa hip-hop nchini Frida Aman ameonesha maumivu yake juu ya suala hilo na ameomba kufanyika njia ya usawa wa kijinsia. "Yaani tuone mtu akibakwaaa halafu tuambiwe aliyebakwa alikuwa anajiuza kwanini tutafute njia ya kuonesha alichofanyiwa ni sawa jamani hii leo imeniumaa sana,"ameeleza.


Mbali na hao mastaa wengine pia kama vile Kajala Masanja, Meena Ally, Jacline Wolper,Rosa Ree, Dj Sinyorita na wengineo wameendelea kuchapisha picha kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii inayoonesha mkono na maneno yasomekayo "'Enough is enough' tunadai haki kwa binti aliyebakwa na kulawituwa".


Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwezi huu zilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii zikionesha binti ambaye jina lake halijawekwa wazi akifanyiwa vitendo vya ubakaji na kulawitiwa na vijana watano na kudaiwa kuwa walitumwa na askari kufanya hivyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad