Mchezaji Vini JR Apiga Chini Ofa ya Trilioni 3 Saudia

Mchezaji Vini JR Apiga Chini Ofa ya Trilioni 3 Saudia



Nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius Jr (24), amekataa ofa ya kihistoria ya €1 bilioni sawa na TZS trilioni 3 kutoka Al-Ahli ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League). Ofa hiyo, ambayo ni mara 13 ya mshahara wake wa sasa, ilihusisha mkataba wa misimu mitano na ingekuwa mkataba mkubwa zaidi katika historia ya michezo.


Ofa hiyo iliandaliwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia, ambao ulilenga kumfanya Vini Jr. kuwa uso wa ligi hiyo kuelekea Kombe la Dunia la 2034, ambalo Saudi Arabia inatarajia kuandaa. Pamoja na mshahara huo wa kuvutia, ofa hiyo ilijumuisha fursa ya kuwa mchezaji huru mwaka 2029, nafasi ya kurejea Ulaya kabla ya kufikisha miaka 30, na nafasi yoyote ya kazi katika soka la Saudi baada ya kustaafu.


Hata hivyo, Vini Jr ameamua kubaki Real Madrid, na malengo yake ya kufikia mafanikio makubwa kwenye soka la Ulaya, ikiwa ni pamoja na kutwaa tuzo ya Ballon d’Or.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad