Miili 9 yafukuliwa kwa mganga, vifo vyafika 10

 

Miili 9 yafukuliwa kwa mganga, vifo vyafika 10

Jeshi la Polisi limesema baada ya kuendelea na uchunguzi na mahojiano kuhusu vifo vya Watu watatu ambao miili yao imefukuliwa nyumbani kwa Mganga wa kienyeji aitwaye Nkamba Kasubi Mkoani Singida, hatimaye jana August 27,2024 Mganga huyo alikubali kuwaongoza Polisi hadi kwenye Mji wake mwingine uliopo Kijiji cha Porobanguma, Tarafa ya Kwamtoro Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma na kuonesha mashimo mengine sita ambayo walifukia Watu wengine wakiwemo Watoto waliowaua na kuwazika na kufanya miili iliyofukuliwa kwa Mganga kufikia tisa huku mwili mwingine wa 10 ukiokotwa porini.


Taarifa iliyotolewa leo August 28,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema “Baada ya taratibu za ufukuaji kufanyika ilipatikana miili ya Seni Jishabi (28), Mkazi wa Kijiji cha Porobanguma ambaye alipotea toka March 3, 2024 na walidai kumuua na kumzika April 2024, Mohamed Juma (27), Mkazi wa Nyamikumbi A Mkoa wa Singida ambaye alipotea May 15, 2024 na wao wameeleza walimuua kwa kumnyonga kisha kumzika, Daudi Msanku (27), Mkazi wa Gawidu Mkoani Manyara ambaye alipotea May 27, 2024 na baada ya kumuua walichoma mwili wake moto kisha majivu yake kuyahifadhi kwenye ndoo, huyu ndiye ambaye pikipiki yake alikamatwa nayo Miraji Shabani Nyalandu akijaribu kutoroka baada ya kuona Watuhumiwa wenzake wanakamatwa mfululizo na Askari Polisi”


“Mwingine ni Ramadhan Yusuph (26), Mkazi wa Kidika Mkoani Manyara, ambaye walimuua April 2024, Mwekwa Kasubi (umri miezi 4), Mttoo huyu ni wa huyo Mganva wa kienyeji ambapo aliuawa March 2023, Maka Selemani Shabani Nyalandu (umri miezi miwili), aliuawa June 2023 na ni Mtoto wa muhumiwa Selemani Shabani Nyalandu maarufu Hango, Watoto hawa walizikwa wakiwa hai kwenye zizi la mifugo, pia Watuhumiwa walikiri kumuua Ramadhani Bakari Kilesa (80), Mkazi wa Porobanguma na kutupa mwili wake katika Pori la Akiba Swangaswanga, maiti yake ilipatikana July 25, 2024 lakini ilikuwa haijabainika kuwa aliuawa na Watuhumiwa hawa hadi jana walipokiri kumuua na kueleza sehemu walipomtupa ili mwili wake uliwe na wanyamapori”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad