Baadhi ya mashabiki wa Klabu ya Yanga jana walilazimika kuingia katika uwanja wa Uhuru kufatilia tukio la kihistoria la #YangaDay kupitia "Big Screen TV" iliyofungwa katika uwanja huo baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kujaa.
Akizungumzia tukio hilo, Mchambuzi wa masuala ya michezo kutoka TV3, Alex Ngereza amehoji kuhusu mashabiki hao ni wapi walipata tiketi hizo za kuingia Dimba la Uhuru kama tiketi zinauzwa mtandaoni na tamasha lilikuwa likifanyika Uwanja wa Mkapa.
"Mimi nimejiuliza wale mashabiki ambao waliingia uwanja wa uhuru tiketi walizipata wapi? Kama tiketi ziliuzwa zote na tupewa taarifa kwamba tiketi zimeisha je wale mashabiki ambae waliweka uhuru tiketi zilitoka wapi?
"Kama kungekuwa na ongezeko la tiketi wangetangaza kwamba tiketi zimeisha lakini Kuna ticket ambazo ukinunua utaingia wa uhuru na kutakuwa na big screen.
"Kama wale walikuwa na tiketi na amepelekwa uwanja wa uhuru basi Kuna makosa yamefanyika, hakukuna na tangazo sehemu yoyote kwamba Kuna tiketi za ziada kwa ajili ya watu kuingia uwanja wa uhuru, amesema Alex Ngereza.