MUDATHIR wa Yanga Aanza Kupigiwa SIMU za Ulaya Mapema Sana

MUDATHIR wa Yanga Aanza Kupigiwa SIMU za Ulaya Mapema Sana


 MZEE WA KUPIGA SIMU MUDATHIR Yahya kiungo wa Yanga ubora wake ni ule ule unaendelea msimu wa 2024/25 kwa mujibu wa Maulid Kitenge ameweka wazi kuwa kwa Muda simu zitaita sana.

Agosti 4 katika utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi cha Yanga msimu wa 2023/24 kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 2-1 Red Arrows alipachika bao moja.

Dakika ya 64 aliweka usawa bao la Red Arrows ambalo lilifungwa kipindi cha kwanza kupitia kwa Ricky Banda dakika ya 5 kwa mabingwa wa Kagame Cup.

Bao la pili la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Aziz Ki dakika ya 90 kwa pigo la penalti baada ya beki wa Red Arrows kumchezea faulo Nickson Kibabage.

Kwa Muda simu zitaita sana kwa kuwa msimu uliopita ziliita ni mwendelezo wa furaha.” Kitenge.

Ipo wazi kuwa kwenye Wiki ya Mwananchi iliandikwa rekodi ya kujaza viwanja viwili kwa mpigo kwa mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza kushuhudia tamasha hilo la sita kwa Yanga.

Uwanja wa Mkapa ilikuwa Full House na Huku pia Uwanja wa Uhuru uliingiza mashabiki wa Yanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad