Mukwala Akuna Kichwa na Kusema "Nina Deni Kubwa Sana Simba"



Mshambuliaji mpya wa Simba, Mganda Steven Mukwala hajawapa furaha Wanamsimbazi, lakini mwenyewe amekiri sasa anauona ukubwa na thamani ya kikosi hicho baada ya kuanza kukitumikia tangu ajiunge msimu huu akitokea Asante Kotoko ya Ghana.
.
Mukwala alisema tangu atue nchini amekutana na presha kubwa kuanzia katika benchi la ufundi hadi kwa mashabiki, jambo ambalo ni tofauti na baadhi ya klabu alizochezea ingawa anaendelea kuzoea mazingira.
.
“Kila mmoja anaweza kuongea kadri anavyoweza kwa sababu huwezi kuzuia hilo. Natambua bado nina deni kubwa la kufanya ndani ya timu hii ili kufikia malengo, hivyo siwezi kusikiliza maneno ya watu kutokana na kutofanya vizuri,” alisema Mukwala.
.
Nyota huyo aliongeza, jambo kubwa linalompa matumaini makubwa ya kufanya vizuri msimu huu ni kutokana na imani kubwa ya kucheza anayoendelea kupewa na benchi lao la ufundi la timu hiyo, chini ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Fadlu Davids.
.
“Mashabiki siku zote wanapenda mambo mazuri na siwezi kuwaahidi jambo lolote zaidi ya kuomba ushirikiano wao, suala la kutofunga natambua linawaumiza wengi, ila nalichukulia kama changamoto ambayo inanifanya nipambane zaidi ya sasa,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad