Mume Atumia Drone Kumnasa Mke Wake Akichepuka Na Bosi Wake Kwenye Pagala

 

Mume Atumia Drone Kumnasa Mke Wake Akichepuka Na Bosi Wake Kwenye Pagala

MWANAUME mmoja nchini China hivi karibuni alimnasa mkewe akichepuka na Bosi wake wakati wa kazi, kwa kutumia Ndege isiyo na rubani (Drone)


Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Jing (33)  alianza kumshuku mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje baada ya mwanamke huyo kubadilika tabia jambo lililomfanya kuanza upelelezi.


Jing aliamua kutumia ndege isiyo na rubani kumpeleleza mke wake kwa umakini mkubwa huku akihakikisha hakuna atakayegundua anachokifanya.


Siku moja kwenye upelelezi wake alimwona mke wake akitoka ofisini na mtu asiyeeleweka na kuingia naye kwenye gari.


Waliondoka kwa gari hadi eneo la mbali la Milimani ambapo ndege isiyo na rubani iliwakamata wakiwa wameshikana mikono na kuelekea kwenye Nyumba mbovu iliyojificha. Dakika 20 baadaye, wawili hao walitoka nje ya nyumba na kurudi Kazini


Jing baadaye aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kuripoti kwamba mwanamume aliyenaswa kwenye video na ndege yake isiyo na rubani alikuwa Bosi wa mkewe, na kuchapisha picha zao wakiwa wameshikana mikono na kusema angetumia picha hizo za ‘Drone’ kama ushahidi wa kupata Talaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad