Muonekano wa Vybz Kartel yazua Hofu kwa Mashabiki

 

Muonekano wa Vybz Kartel yazua Hofu kwa Mashabiki

Mwanamuziki maarufu wa 'Dance Hall' kuoka nchini Jamaica Vybz Kartel ameendelea kuwatia moyo mashabiki zake kuwa atarejea kwenye hali yake ya kawaida licha ya kuonekana kuzorota kiafya baada ya kutoka jela ambapo alikuwa na hali mbaya ya kiafya inayotishia uhai wake kama vile (Graves’ Disease) maradhi ya kutisha kwenye Koo na Moyo.


Vybz alikuwa jela nchini Jamaica tangu 2011 alipokamatwa kufuatia kutoweka kwa mshirika wake Clive “Lizard” Williams, ambaye mwili wake haujawahi kupatikana.


Kartel alihukumiwa kifungo cha maisha jela machi 13, 2014 baada ya kukutwa na hatia na mauaji ya Clive ‘Lizard’ Williams yeye pamoja na wenzake watatu ‘Shawn Campbell’, Andre St John na Kahira Jones na kuachiwa huru Julai 31, 2024.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad