Nchimbi Aagiza Viongozi wa Chadema Waliokamatwa Mbeya Waachiwe


Nchimbi Aagiza Viongozi wa Chadema Waliokamatwa Mbeya Waachiwe

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo kuwaachia huru Viongozi wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wanaoshikiliwa na Polisi Jijini Mbeya.


Dr. Nchimbi ametoa agizo hilo katika Mkutano uliofanyika Wilayani Geita wakati akizungumza na Wakazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro, Geita ambapo ameuelekeza Naibu Waziri Sillo kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ili Viongozi hao wa CHADEMA waachiwe huru.


“Kwakuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani upo hapa, mambo ya sheria sio ya kutolea maelekezo Kiongozi wa Chama cha siasa lakini nitumie nafasi hii mwambie Waziri wako kwamba tunaomba muone uwezekano wale Viongozi wa Vyama vya siasa waachiliwe ili mtupe nafasi ya kuzungumza nao kwasababu tunajenga Taifa moja tunapenda kuwa na Taifa tulivu kama kuna maeneo wamekosea wao au tumekosea sisi tukae tuzungumze tuijenge Nchi yetu” ——— Dr. Nchimbi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad