Nchimbi Atoa Maagizo Kwa Mawaziri Wanne

Nchimbi Atoa Maagizo Kwa Mawaziri Wanne


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa maelekezo kwa Mawaziri wanne kufuatia maombi ya Wananchi wa Mwandiga Mkoani Kigoma kuhusu umeme, usalama wa raia na mali zao, maji na kituo cha afya.


Balozi Nchimbi ambaye yuko Kigoma akiendelea na ziara yake ya siku 3 Mkoani humo, aliyoanza Agosti 4, 2024, ametoa maelekezo kwa Wizara hizo alipokuwa akiongea na Wananchu wa Mwandiga, Jimbo la Kigoma Kaskazini, aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Kasulu.


Maelekezo ya kwanza ya Balozi Nchimbi yameelekezwa kwa Waziri wa Nishati, akiitaka Wizaea hiyo iongeze kasi katika kusambaza umeme kwenye ngazi ya vitongoji baada ya kumaliza vijiji vyote Nchini na pia amemwelekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhakikisha kinajengwa kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao eneo la Mwandiga na maeneo mengine ya jirani jimboni humo, ambapo wameonesha uhitaji huo kupitia mabango yao wakati wakimpokea Katibu Mkuu huyo wa CCM, pia kutokana na maombi ya Mbunge wao, Assa Makanika alipokuwa akizungumzia maendeleo ya Jimbo hilo kwenye mkutano huo.


Vilevile, Katibu Mkuu wa CCM ametoa maelekezo kwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), aliyewakilishwa na Naibu Waziri Zainabu Katimba, akimwelekeza afikishe maelekezo hayo kwa Waziri, kuhusu mahitaji ya kujengwa kwa Kituo cha Afya kwa ajili ya Tarafa ya Mwandiga.


Maelekezo mengine ya Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameyaelekeza kwa Wizara ya Maji, kutokana na Wananchi kumpatia taarifa kuwa mtandao wa maji hautoshelezi mahitaji kulingana na idadi ya Watu katika eneo hilo la Mji Mdogo wa Mwandiga “Waziri wa Maji atatakiwa kuja huku kwa haraka afanyie kazi suala hili na akifika huku Kigoma apite hapa Mwandiga pia kuangalia ufumbuzi wa suala hili la mtandao wa maji maeneo haya ili tumalize hii changamoto huku Kigoma Kaskazini”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad