Rais Dk. Samia Kuzindua Mradi Wa Reli Ya Umeme Dar Es Salaam Hadi Dodoma

 

Rais Dk. Samia Kuzindua Mradi Wa Reli Ya Umeme Dar Es Salaam Hadi Dodoma

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 1, 2024 anatarajiwa kuzindua mradi wa reli ya kisasa ambao umeanza safari zale DAR-DODOMA huku kiasi cha Dola bilioni 3.138 kikiwa kimetumika katika ujenzi huo kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma ikiwa ni jumla ya kilometa 722, ikiwa ni sehemu, ya awamu ya kwanza ya ujenzi huo kukamilika na kuanza kutoa huduma.


Safari ya kutoka DAR-MOROGORO hutumia saa moja na dk 45 huku kutokea DAR ES SALAAM hadi DODOMA hutumia Saa Tatu na dk 25, huku ikiwa na uwezo wa kubeba tani 10 za mizigo sawa na malori 500.


Viongozi mbalimbali watashiriki uzinduzi huo akiwemo Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi.


Lengo la reli hii ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa;


Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo.

Uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.

Oboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayo pitiwa na mradi.

Kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.

Faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.

Rais Dk. Samia Kuzindua Mradi Wa Reli Ya Umeme Dar Es Salaam Hadi Dodoma


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad