Rais Samia aagiza kurejeshwa kwa huduma za Kijamii Ngorongoro

 

Rais Samia aagiza kurejeshwa kwa huduma za Kijamii Ngorongoro

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ikiwemo za elimu na afya zilizokuwa zimesitishwa katika Tarafa ya Ngorongoro.


Hayo yamesemwa leo Ijumaa Agosti 23, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku 5 wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.


Aidha amesema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama unavyofanyika maeneo mengine nchini

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad