Rais Samia Suluhu "Kuagiza Sukari nje ya Nchi ni Kupoteza Fedha"

Rais Samia Suluhu "Kuagiza Sukari nje ya Nchi ni Kupoteza Fedha"


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara kuvipa kazi viwanda vya ndani ya Nchi ikiwemo Kilombero Sugar ili vizalishe sukari ya majumbani na viwandani na ethanol kwa ajili ya nishati ya kupikia huku akisema kuagiza tani 250000 ya sukari nje ya Nchi kwa ajili ya viwanda ni matumizi mabaya ya fedha.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo August 04,2024 baada ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanda cha sukari Kilombero-K4 Mkoani Morogoro.

“Niwaelekeze Mawaziri wawili wa Kilimo na wa Biashara, katika mahitaji yetu ya sukari Nchini, nimeambiwa tani 650000 ni matumizi ya sukari tunayotumia majumbani lakini viwanda vinahitaji tani 250000, sasa tani 250000 tukiendelea kuagiza ni upotevu wa fedha za kigeni”

“Mimi nina uhakika tukivipa kazi viwanda vyetu vinaweza kutuzalishia sukari ya viwandani, kwa hiyo sasa hiyo ndiyo kazi ninataka mkaitekeleze, angalieni mtawekaje sera zetu ili viwanda hivi viweze kuzalisha sukari ya viwandani lakini pia waweze kuzalisha ethanol kwa ajili ya kupata nishati safi ya kupikia na kwa matumizi mengine”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad