Rais wa TLS Mwabukusi Aanza Kazi Kwa Kasi ya SGR.....


Zikiwa zimepita siku tatu tangu Boniface Mwabukusi achaguliwe kuwa rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ameanza kazi kwa kujitosa katika sakata la msichana anayedaiwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kisha video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Video hiyo iliyoanza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana Agosti 4, 2024 ikidaiwa msichana huyo amebakwa na kulawitiwa na vijana watano.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na TLS na kusainiwa na Mwabukusi leo Jumatatu Agosti 5, 2024 imesema chama hicho kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa sakata hilo, ili kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mwabukusi kutoa taarifa rasmi kwa umma tangu aapishwe kuwa rais wa TLS Jumamosi ya Agosti 3, 2024.

“Tukio hilo sio tu ni kinyume na sheria za nchi yetu, lakini pia ni kinyume na maadili na utamaduni wetu kama Watanzania. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinalaani kitendo hiki kiovu na tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kisheria na kuhakikisha wahalifu wote waliotenda kitendo kile na waliowezesha kutendwa kwa kitendo kile kiovu wanakamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja, ili haki itendeke.

“TLS inapinga vitendo vyote vya kikatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya usalama na haki jinai kuhakikisha wahalifu hao wanafikishwa katika mamlaka sahihi za haki, ili kujibu mashitaka yao,”imeeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad