Zikiwa zimesalia siku 3 kuelekea siku ya Simba Day ‘UBAYA UBWELA’ tarehe 3 August klabu hiyo imeendelea kufanya vyema kwenye mauzo yake ya tiketi. Taarifa zilizotolewa na klabu hiyo kuhusu mwenendo wa mauzo ya Tiketi umeonyesha kwamba tiketi za PLATINUM NA VIP A zimekwishamalizika. Tiketi za VIP B zimefikisha asilimia 86, mzunguko asilimia 88, VIP C asilimia 65 na Machungwa ni asilimia 57.
Afisa habari wa klabu hiyo amenukuliwa akisema .Maandalizi ya Simba day yanakwenda vizuri kama mnavyoona na tunaamini tiketi zitamalizika kabla ya tarehe husika,tiketi za platnum na vip a zimemalizika mapema sana hivyo shabiki hakikisha hukosi hizo tiketi nyingine ‘
Katika siku hiyo ya Simba Day yatafanyika mambo mengi lakini linalosubiriwa kwa hamu ni utambulisho wa nyota wapya waliosajiliwa kuelekea msimu wa 2024/25 utakaoanza kutimua vumbi tarehe 8/8 . kwa upande wa burudani Simba wametoa orodha ya wasanii watakaotumbuiza siku hiyo akiwemo alikiba,Joh Makini,dula makabila na Chino.
Kwa upande wa kikosi
Kikosi cha Simba kilichokuwa kimeweka kambi jijini Isimailia nchini Misri kimeshawasili jijini Dar es salaam kujiandaa na siku hiyo muhimu huku mchezaji wao Kibu Denis akikosekana katika msafara huo kutokana na kutojiunga na kambi ya timu.
golikipa Ayoub Lakred yupo kikosini lakini atalazimika kukosa mechi za awali kutokana na majeraha aliyonayo na anatakiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki 4 mpaka 6 .taarifa zisizo rasmi zinasema Simba wako mbioni kumsajili golikipa Moussa anayekipiga Hroya FC ya Guinea ili kuziba pengo la Ayoub