Baada ya kipigo cha tatu mfululizo cha bao 1-0 kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii, miongoni mwa mashabiki wa Simba SC wamekubali ubora wa watani zao, Yanga kutokana na kikosi chao kilivyo hivi sasa.
Msimu uliopita kutoka na udhaifu wa kikosi cha Simba tulikosa "CLASSIC MATCH" baina ya timu hizi ila msimu huu imeonekana dalili njema kuelekea Derby zijazo.
Kocha wa Simba alisema wachezaji wake bado hawajawa tayari kucheza dakika 90 ndicho kilichoonekana leo, Wachezaji ambao walikua wanakimbia sana mwanzoni walichoka mapema sana kabla mpira haujaisha mfano wa haraka ni Mutale na Deborah.
Debora anajua mpira ila Pumzi yake imemsaliti, Duke Abuya ni mfia timu haswa kaivuruga sana Simba katikati na kumpa mechi rahisi sana Aucho.
Ile draft iliochezwa bao la Max Nzengeli Daah! Lile bao limetokea Uwanja wa mazoezi Chamue Karaboue ni beki mzuri sana na mgumu mno, Ule ukuta wa Yanga Bacca na Job umefanya tena kazi ya kiume katika mechi dume.
Yanga wamenyimwa bao halali (Aziz Ki) na Simba SC wamenyima Penati halali (Kijili) Refa anajua zaidi alichokifanya na huu utabaki kua mtazamo wangu mimi Ayubu Taarifa.
Agustine Okejepha aliituliza sana Timu na ilicheza katika mamlaka yake jukumu aliloshindwa Mzamiru, Ila yule Yao ni mbishi sana ila amepewa mechi ngumu na Mutale leo na hajaonekana kabisa kwenye mstari wa kushambulia.
Desse Mukwala kama anakuja halafu anakataa, Dakika 90 hajalishwa mpira wowote wa maana Siwezi kumuhukumu yeye kama Striker hajapewa huduma , Pacome Peodoh Zouzoua ni kiungo mshambuliaji anaeweza kufanya recoveries Timu yake inapopoteza mpira na hapa ndio anajitofautisha na Viungo wengi.
Yanga wameshinda mechi, Simba wameepuka lawama kwa mashabiki wao huwezi kuona mti analaumiwa moja kwa moja kwa matokeo haya wengi wamekubali fighting spirit level ya vijana wao. Bonge la mechi, Hongereni sana Yanga. Imetuuma lakini hatujatumia.
kauli ya shabiki wa Simba