Tanzia: Mwimbaji Marko Joseph wa Zabron Singers afariki Dunia

Tanzia: Mwimbaji Marko Joseph wa Zabron Singers afariki Dunia


Mwimbaji wa kundi la Zabron Singers, Marco Joseph amefariki dunia kwa ugonjwa wa Moyo jana usiku Agosti 21, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika taasisi ya Moyo (JKCI) Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Shemeji wa marehemu, Tecla Lucas amesema leo kuwa mwili wa marehemu bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali hiyo, wakisubiri ratiba za mazishi kupangwa.


"Amefariki kwa ugonjwa wa moyo akiwa Hospitali ya Muhimbili jana usiku msiba utakuwa Mikocheni kwa mama yake mdogo, mwili kwa sasa bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti," amesema Tecla.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kwaya ya Zabron Singers, Japeh Zabron amesema kaka yake alipata mshtuko wa Moyo wakati Wakiwa safarini kihuduma nchini Kenya siku chache zilizopita.


Jitihada za matibabu zilifanyika katika Hospital ya rufaa Bugando lakini alipewa rufaa kwenda JKCI kwa matibabu zaidi kabla ya kufariki akipatiwa matibabu.


Miongoni mwa nyimbo alizotamba nazo akiwa na Kundi hilo ni Mkono wake Bwana, Swetie Sweetie, Sisi Ndio Wale, Uko Single, Nakutuma Wimbo na nyingine nyingi.


TanzaniaWeb TV inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na mpendwa wao.


Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad