Uchambuzi YANGA Vs SIMBA, Kiufundi ilikuwa hivi

 

Uchambuzi YANGA Vs SIMBA, Kiufundi ilikuwa hivi

Mechi bora mno kimbinu na kiutekelezaji! ‘Tactical awareness’ ya wachezaji ilikuwa kubwa na ilivutia kutazama. Nimependa mpangilio wa wachezaji ndani ya maeneo muhimu ila kitu tulichonyimwa ni magoli mengi.


Yanga wameshinda kwa ustahiki! Hawakukaa sana na mpira ila walichagua kukimbia na mpira kwa muda fulani na kushambulia kwa idadi ndogo ila wakiwa hatari (Economy speed and transitions). Kuna namna wanaenjoy kucheza kwa sababu kila mtu anamjua vyema.


Simba!? Kiwango bora na maimarisho muhimu mno! Nilipenda wachezaji walivyoutaka mpira haraka wanapoupoteza na wanavyofika haraka kwenye maeneo magumu! Uchezaji wao ulikuwa mzuri na kitu pekee walichokosa ni urahisi wa washambuliaji kufunga kwa sababu nafasi zao nyingi zilikuwa 50/50.


Dickson Job ndiye Man of the Match wangu by the reasons! Amefanya tackling 4 za kuamua mechi. Ni sehemu ambazo angezubaa Yanga walikuwa wanaumia! Akili kubwa na wepesi wa kutii mbinu.


Asante Karaboue. Nimefurahi utulivu wake na tabia halisi za mabeki wa kati… Juu yupo, chini yupo na uwezo wa kutuma wenzie ulikuwa vyema.


Yule Pacome wajameni Unafurahia kila kitu kwake. Uelewa wake wa mchezo ni wa juu mno. Counter Simple build up Ni bahati tunamuona kila weekend nchini kabla haijawa too late.


Debora Fernandez just Calm Mpira sio vita. Alichoshwa kipindi cha kwanza na ukabaji dhaifu wa Mzamiru na hata alipojipata alishachelewa! Amecheza vizuri sana.


Another day of Aucho Anajua sana kulinda ukuta wake na leo kacheza kiungwana sana. Kuna salama nyingi za Yanga kwake!


Fine match Che Malone, Zimbwe na Okejepha. Mukwala?! Very hunter Boka, Yao alaf kuna yule Maxi Mpia… Ni ngumu kumkaba.


Mwanzo mzuri kwenye maendeleo ya Simba! Tusubiri mwendelezo na wachezaji wengi wametoa kilicho bora! Waamuzi huwa sizungumzii walichokifanya!


1. Fadlu Davids (Arteta wa Bongo) Ametoa game bora sana mbele ya Master Gamondi. Hakuingia kinyonge, alipishana vema sana na Yanga Sc, Ni vile wachezaji wake walikosa ufanisi katika final third lakini mechi ingeweza kuwa na both team to score (GG).


2. Simba SC matumizi ya inverted wings bado ni changamoto. Mutale mzuri mno akiwa na mali mguuni lakini end products yake ni poor, Balua hakuonekana kuwa katika maeneo muhimu wakati timu inashambulia.


3. Kiungo cha Simba Sc bado kuna vitu havipo sawa, Pamekuwa na mistake nyingi, Wanapoteza mali kirahisi sana, at least mabadiliko ya Ngoma na Augustine yalienda kuweka utulivu katika base ya midfielder.


4. Yanga Sc gia yao iko pale pale (Namba tano) wanawasha na kuondoka, Wamekamilika sana kimbinu bila mpira wanazuia vema sana, Wakiwa na mpira wapo sharp kushambulia ngome ya wapinzani.


5. Paccome kila kitu kafanya kwa umahiri wa hali ya juu sana, Alikuwa na mechi boro sana, Kama ni alama kiurahisi anachukua 9/10, Ibrahim Bacca wala haishangazi maana tuzo ya beki bora ipo kabatini kwake. Perfomance bora sana kwa ushirikiano wa karibu na Dickson Job.


6. Macho yako yameona nini kwa golikipa Djugui Diarra, Kuna namna kama vile mipira mirefu (Long bolls) ilikuwa inamkataa kiaina. Mudathir Yahya game change wa Gamondi, Baada ya kuingia yeye alienda kuweka utulivu eneo la katikati kwa upande wa Yanga. Ila birthday boy AUCHO ile faulu dhidi ya Mutale ndo maana halisi ya kadi ya timu.


NB. Nasikia Ally Kamwe kashafika Ferry anaelekea Kigamboni kuchukua Mke


UBAYA UBWELA UMEKUWA UBAYA UBAYA TU


Mechi ambayo Physically ilikuwa inachosha sana, kila mchezaji alikuwa ana sprint sana , pressing runs yaani hakuna muda wa kupumzika: Yanga hasa kipindi cha kwanza licha kupata goli walicheza kwa intensity ya kati sana katika lines zote tatu


Ambapo Simba walidominate katika kushinda mipambano yao kuanzia nyuma katikati na kupitia pembeni mara nyingi sana (Fernandez, Mutale, Balua , Mukwala ) walikuwa wanapressing vya kutosha lakini Yanga wao walikuwa imara zaidi katikati ( Abuya , KI Aziz , Nzengeli , Pacôme ) walikuwa wafanisi katika kupiga one touch football kupitia katikati ambapo kwa Simba ilikuwa viseversa


Kwa upande wa Simba nilichokipenda zaidi ni jinsi Fadlu Davids alivyowapika wachezaji kuweza kushinda mipambano yao , na walikuwa wanazuia vizuri sana ( yani kutumia vizuri ile PPDA ) , kwa maana walikuwa wanamruhusu Yanga wachezs pasi chache na kufika : tatizo la Simba lilikuwa ni kuunganisha safu ya kiungo ( katikati ) kwenda kwenye eneo la mwisho ( Mukwala etc )


Miguel Gamondi alijua jinsi ya kucheza na Simba ni kupiga one touch football kwanini? Ili kuimove shape yao ya ulinzi kwa haraka sana licha ya Simba kuwa na Pass Per Defensive Action nzuri (ndicho kilichotokea), ile combination play ya Nzengeli, Pacôme, KI Aziz plus Dube ukiwaachia space na time ni lazima wakuadhibu : Nzengeli ghafla. Bang (goal) wavuni.


A VERY GOOD MATCH KWA YANGA & SIMBA KWA HAKIKA WAMETUPA MECHI NZURI SANA


1: Nzengeli aisee anajua sana kuusoma mchezo, unaweza usimuone sana uwanjani lakini kwenye matukio muhimu utamuona, good goal


2: Mutale ni mchezo mzuri sana, yani anacheza kushoto, kulia, katikati kwa kiwango kikubwa


3: Pacôme huyu jamaa unaweza kumuongelea vyovyote unavyotaka, ni brain ya football.


4: Wachezaji wa Simba wamecheza vizuri licha kupoteza mechi, kuna kitu kimeingia kutoka uwanja wa mazoezi, wanaendelea kuimarika.


5: Yanga wamecheza vizuri zaidi, utulivu kwenye kufanya maamuzi sahihi, top top team wanajua jinsi ya kupunguza makosa


6: Yule Mwamuzi wa kati aisee, alikuwa na poor decisions


7: Fainali ileeeeeeee!!!


FT: Young Africans 1-0 Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad