Uchambuzi: Yanga Walifanikiwa Hapa Kuwaangamiza Vital'O

 

Uchambuzi: Yanga Walifanikiwa Hapa Kuwaangamiza Vital'O

Young Africans imeibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Vital’O katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali na kufuzu kwa kishindo hatua inayofuatia.


Mabao ya Pacome Zouzoua dakika ya 14 kwa penalti, Clement Mzize (dk 49), Clatous Chama (dk 51), Prince Dube (dk 71), Aziz Ki (dk 78) na  Mudathir Yahya (dk 86) yalitosha kufanikisha ushindi huo.


Tangu mwanzo wa mchezo, Young Africans walionekana kuitaka mechi kwani mashambulizi ya hapa na pale yalimlazimisha beki wa Vital’O kuushika mpira makusudi uliokuwa unaelekea nyavuni, akaonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 12.


Ushindi huo unaifanya Young Africans kufuzu hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 10-0 baada ya mchezo wa kwanza kushinda 4-0.


Baada ya kufuzu hatua ya kwanza, sasa Young Africans inakwenda kucheza dhidi ya CBE ya Ethiopita katika mchezo wa kuwania kuingia makundi.


Mchezo wa kwanza Young Africans itaanzia ugenini kati ya Septemba 13 na 15, kisha marudiano ni kati ya Septemba 20 na 22 mwaka huu.


YANGA HII UNAIFUNGAJE


Yanga SC wamepiga dominance, walitawala kila idara dhidi ya Vital'O, kama kungekuwa na sheria za kutupa taulo ili game imalizike basi Vital’O walikuwa wanafanya hivyo haraka sana, why ? Ilikuwa ni kuangalia Yanga wanafunga ngapi?


Hata ukicheza mchangani siku zote ukifanya mistakes (makosa) mengi, upo matatizoni kupoteza mechi, na unapoteza kwa magoli mangapi na dhidi ya nani? Maana yake dhidi ya mpinzani amabye ni hatari, utaokota nyingi golini (ndicho Vital'O kilichowakuta) kwanini?


1: Kulikuwa na Distance kubwa sana katika mistari yote mitatu (Ulinzi, Kiungo, Ushambuliaji), iliwapa ugumu sana kuzuia na kushambulia (Vital'O) kwasababu walikuwa mbalimbali sana


2: Kulikuwa spaces kubwa sana katika mistari ya Kiungo na Ulinzi


3: Recovering zilikuwa hazipo imara sana


Ukicheza hivyo dhidi ya Yanga SC na huzingatii (SPACE and DISTANCE), na haupo compact kwa maana ya kubana zaidi / kuwa finyu yani utapata ulichokitaka, Vital’O vile walivyohitaji havikufanikiwa why? Yanga walikuwa imara sana kila idara (attacking and defending), quality quality quality.


NOTE


1: TRIPLE C .. CHAMA - unaweza kumuelezea vile unataka, anajua sana ball na hana uchoyo kabisa yani assists anazipenda sana na anazipatia mno.


2: MZIZE ..... i see you champs.


3: Vital'O nafikiri wameshukuru sana hata hizi 6 tu maana zingeweza kufika hadi 8 au hata 9 dah.


4: Wachezaji wa Yanga wamecheza vizuri sana ... kila mmoja ametoa jasho la maana kabisa


5: Hivi Yanga hamtosheki na magoli? Hela za Mama mnataka kuzimaliza na kuna Supu kesho?


FT: Yanga SC 6-0 Vital'O.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad