WAAMUZI MCHEZO WA YANGA NA SIMBA LEO 08 AUGUST 2024

WAAMUZI MCHEZO WA YANGA NA SIMBA LEO 08 AUGUST 2024

 WAAMUZI MCHEZO WA YANGA NA SIMBA LEO 08 AUGUST 2024

Ikiwa imesalia masaa pekee kabla ya mtanange mkali wa Kariakoo Derby baina ya Yanga na Simba katika mashindano ya kumsaka bingwa wa Ngao ya Jamii 2024, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi waamuzi watakaochezesha pambano hilo la ambalo limekua likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa soka.


Katika mchezo huu, Yanga na Simba zote zinaingia uwanjani zikiwa na kiu ya ushindi. Wachambuzi wa soka wanatabiri mechi kali na yenye ushindani mkubwa kama ilivyo zoeleka pale timu hizi mbili zikikutana. Yanga watakuwa wakitegemea makali ya Stephan Aziz Ki na Pacomewakati Simba wakijivunia uwezo wa Jean Charles Ahoua na Joshua Mutale.

Elly Sasii Aongoza Jopo la Waamuzi Mahiri

Elly Sasii, mwamuzi mwenye uzoefu mkubwa na sifa za kusimamia mechi kubwa, amepewa jukumu la kuchezesha mchezo huu muhimu utakaofanyika Agosti 8, 2024, Uwanja wa kimataifa wa Benjamin Mkapa. Sasii anatarajiwa kuonyesha umahiri na utulivu wake katika kuhakikisha mchezo unachezwa kwa haki na uwazi.

Ahmed Arajiga Kuchezesha Azam vs Coastal Union

Wakati huohuo, mwamuzi Ahmed Arajiga amechaguliwa kuchezesha mchezo mwingine muhimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Azam FC na Coastal Union. Mchezo huu utafanyika saa 10 jioni katika Uwanja wa Aman, siku hiyo hiyo ya Agosti 8.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad