Wananchi Wamchangia Wakili Madeleka Kwenda Kortini Kesi ya ‘Afande’

 

Wananchi wamchangia Wakili Madeleka Kwenda Kortini Kesi ya ‘Afande’

Baadhi ya watu wamejitolea kumchangia fedha Wakili Peter Madeleka na wenzake kusikiliza kesi dhidi ya Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Fatma Kigondo, wanayemtuhumu kutuma vijana kubaka na kulawiti binti anayedaiwa mkazi wa Yombo Dovya, wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam.


Kesi hiyo ilifunguliwa Agosti 20 mwaka huu na Wakili Paul Kisambo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma na kupewa namba 0000058901 kwa tuhuma za kumfanyia ukatili wa kijinsia binti huyo na video yake kusambazwa kwenye mitandao kijamii.


Kupitia ukurasa wake wa X, Wakili Madeleka aliarifu umma kuwa kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa leo na kuwaomba Watanzania wachangie gharama za usafiri wa mawakili wataokwenda kusimamia kesi hiyo kwa upande unaoshtaki.


Saa moja baadaye, Wakili Madeleka aliweka ujumbe kuwa kuna uwezekano mkubwa atashindwa kusafiri kwenda Dodoma kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo kutokana na kukosa fedha.


"Kwa sababu ya kukosa fedha, kuna uwezekano mkubwa kesho nitashindwa kwenda Dodoma kwa ajili ya kesi ya jinai inayomkabili ASP Fatma Kingondo, ngoja tuendelee kumwachia Mungu," aliandika.


Ujumbe huo uliamsha hisia za watu waliomtaka aweke namba ya kuchangia fedha na wale waliokamilisha miamala waliweka risiti kwenye ukurasa wa wakili huo kuthibitisha kuwa wametoa mchango wao.


Tukio hilo liliibuliwa na aliyekuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob wiki mbili zilizopita ambaye aliandika mkasa mzima kwenye ukurasa wake wa X huku akiwatumia nakala Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Ulinzi, Dk. Stergomena Tax na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima.


Baada ya kusambaa kwa taarifa za tukio hilo, Jeshi la Polisi lilikamata vijana wanaodaiwa kutekeleza ukatili huo na kuwapandisha mahakamani, lakini kukawa na shinikizo ‘Afande’ anayetuhumiwa kutuma vijana hao, naye afikishwe kortini.


Mawakili waliojiita "wa haki", akiwamo Madeleka waliamua kumshtaki ofisa huyo wa polisi, wakimhusisha na ukatili huo

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad