Wananchi Wamempata Chama Waliyekuwa Wanamuota?



Baada ya kuishuhudiaYanga SC ikishusha ‘mkong’oto’ wa magoli 6-0 dhidi ya Vital’O pale Azam Complex, Chamazi, kila shabiki wa timu hiyo aliyehojiwa na wanahabari, hakusita kulitaja jina la Chama.

Ni Clatous Chota Chama ambaye tangu atue mitaa ya Jangwani, alionekana kama amepoa hivi. Lakini mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), ‘Mwamba’ huyo wa Lusaka ni kama aliamua kuwakumbusha waliotaka kumsahau.

Mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Agosti 17, Chama alifunga goli moja. Katika mchezo wa jana Chama alifunga goli moja na kutoa ‘assist’ nne.

Kwa matukio hayo, hakika Chama aliwakosha mashabiki wa Yanga na kujikuta hata ukiwauliza hali zao, wanaweza kukujibu ‘Chama yupo salama’

Je, Wananchi wamempata Chama waliyekuwa wanamuota?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad