Washtakiwa Kesi ya Asimwe Wasema Hawajui Kosa lao

 

Washtakiwa Kesi ya Asimwe Wasema Hawajui Kosa lao

Washitakiwa tisa wa mauaji ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuwawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake kisha mwili wake kutelekezwa kwenye karavati katika  kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani kagera wamefikishwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba.


Kesi hiyo namba 17740 ya mwaka 2024  inayowakabili washitakiwa hao tisa wa mauaji ya mtoto Albino Novath Asimwe imesomwa mbele ya hakimu mkazi  wa Mahakama hiyo Elipokea Yona na washitakiwa kusomewa shitaka moja la kuuwa kwa kukusudia.


Mwendesha mashitaka  wa Serikali Erick Mabagala mbele ya Hakimu Yona amesema kuwa waliwasilisha maombi ya  hoja sita katika Mahakama kuu ya kanda ya Kagera na hoja hizo  zilikubaliwa  na Mahakama hiyo.


 


Maombi hayo yaliyowasilishwa Mahakama kuu ni kama ifatavyo.1.Majina pamoja na Anwani zilizopo kwenye maelezo ya mashahidi pamoja na nyaraka hazitowekwa wazi wakati wa usikilizwaji na wakati na mwenendo kabithi (commital).


2.Taarifa/Nyaraka zenye taarifa zote za mashahidi majina na anwani za makazi hazitasambazwa kwa Umma.


3.Maelezo au nyaraka zote zinazoonesha a anuani za mashahidi au ndugu zao hazitatolewa kwa Umma.

4.Kesi itasikilizwa kwa uficho wakati ushahidi utakapokuwa unatolewa.


5.Vinasa sauti wakati wa Usikilizaji wa kesi avitaruhusiwa wakati wa usikilizaji wa   kesi6.Wakati wa mwenendo kukabidhi taarifa za anwani hazitoruhusiwa kutolewa.


Kwa upande wa utetezi wa Mshitakiwa namba moja wa kesi hiyo Elipidius Rwegoshora ukiongizwa na wakili Mathias Rweyemamu umesema wanakubaliana na hoja zilizowasilidhwa mbele ya Mahakama kuu kanda ya Kagera.


Baadhi ya washitakiwa wa kesi hiyo   akiwemo mshitakiwa namba 3,7na 8  wakiwa  wamesimama kizimbani kwa nyakati tofauti walinyoosha mkono mbele ya Hakimu Elipokea nakuhoji kuwa kwa nini wapo Mahakama na wanaendelea kusota rumande?


Hata hivyo mwendesha mashitaka wa Serikali Erick Mabagala alisimama na kuwasomea tena shitaka linalowakabili  uku Hakimu Mkazi Elipokea yona akiwaambia watajitetea pindi kesi  yao itakapoanza kusikilizwa Mahakama kuu.


Washitakiwa wa kesi hiyo  ni pamoja na Elpidius  Rwegoshora, Novat Venant, Nurdin Amada, Ramadhan Selestine, Rwenyagira Burukad Alfonce, Dastan Buchard, Faswiu Athuman, Gozibert Alkard, Dezdery Everinist.


Washitakiwa wote tisa  wamerudishwa rumande Gereza la Bukoba mpaka tarehe 6 Septemba mwaka huu ambapo kesi yao itatajwa tena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad