Watu Wanne Wafariki Dunia Baada ya Scania Kugonga Gari ya Wanafunzi..



WATU WANNE WAMEFARIKI DUNIA WAKIWEMO WANAFUNZI WATATU NA DEREVA... Watu wanne wamefariki dunia wakiwemo Wanafunzi watatu na Dereva mmoja katika ajali iliyohusisha magari mawili ikiwemo Coaster na gari la mizigo aina ya Scania.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo August 31,2024 katika eneo la Gajal Babati Mkoani Manyara ambapo Coaster ilikuwa imebeba Wanafunzi kutoka Hanang kuelekea Mkoani Arusha na baada ya Kufika eneo hilo iligongana uso kwa uso na Scania.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara Ahmed Makarani amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa lori kushindwa kuwa makini barabarani na kuigonga Coaster hiyo iliyokuwa imebeba Wanafunzi 33 wa Shule ya Sekondari Endasaki waliokuwa wakielekea Mkoani Arusha kwa ajili ya likizo baada ya kufunga Shule.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad